SEHEMU YA KWANZA
MAGONJWA SUGU
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya vifo vinavyotokea kila mwaka husababishwa na magonjwa yanayoweza kutibika.
KWA NINI WATU WANATIBIWA MAGONJWA HAWAPONI?
Watu wengi huwa hawaponi kwa sababu mara nyingi madawa wanayotumia yanakwenda kutuliza tu ugonjwa na sio kuondoa chanzo cha ugonjwa. Labda nitumie mfano ufuatao; Ukikata shina la mgomba na kuancha mizizi utakuwa umetoa suruhisho la muda mfupi tu kwani sehemu ya mgomba iliyobaki ardhini huweza kuchepua tena endapo itapata maji ya kutosha. Vivyo hivyo kama usipo ondoa chanzo cha ugonjwa basi ni suala la muda tu ugonjwa huo utarudi tena na tena na tena mpaka hatimae unachukuwa uhai wa mtu husika
CHANZO AU KIINI CHA UGONJWA NI NINI?
Ili kuelewa chanzo au kiini cha ugonjwa, ni vema kwanza ukaelewa nini kinasababisha mwili wako kushambuliwa na magonjwa?
Mwili wa biadamu umeundwa kwa seli mbalimbali. Kuna seli za damu,seli za mifupa,seli za ngozi,seli za kongosho n.k. Kwa ufupi ni kwamba mwili wa binadamu umeundwa kwa mamilioni ya seli ambazo ndio zinaunda organs au viungo tofauti tofauti katika mwili. Seli hizi zinapokuwa sawa bila kuwa na tatizo lolote hufanya kinga za mwili wako kuwa imara na unapokuwa na kinga za mwili ambazo zipo imara basi sio rahisi kwa ugonjwa wowote kushambulia mwili wako na kinyume chake ni kwamba endapo kutakuwa na seli ambayo imechoka au kuchakaa hupelekea kinga za mwili wako kushuka kitendo ambacho hufanya mwili kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa. Kwa hiyo kwa ufupi matatizo yote yanaanzia kwenye ngazi ya seli
TIBU SELI SIO UGONJWA
Unapoona umeshambuliwa na ugonjwa wowote hiyo ni dalili kuwa some how kinga zako za mwili zimeshuka. Kitu muhimu cha kuelewa hapa ni kwamba kitu pekee kinachosababisha kushuka kwa kinga za mwili ni uharibifu katika seli kwa hiyo njia ya uhakika ya kuuondoa ugonjwa ni kutibu seli za mwili wako. Maana yake ni kwamba unatakiwa upate dawa yenye uwezo wa kutibu seli na sio tu kutuliza ugonjwa.
KWA NINI SELI ZINACHAKAA AU KUFA?
Kuchakaa au kufa kwa seli za mwili husababishwa na vitu tofauti tofauti ikiwemo Umri. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu anapotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea kiwango cha uzalishwaji wa seli mwilini hupungua kwa kiasi kikubwa sana. Pia kuna sababu nyingine kama mitindo hatarishi ya maisha kama uvutaji wa sigara,unywaji wa pombe kupindukia na kula sana vyakula vya viwandani. Pia kuna sababu nyingine kama kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi na uzee.
JE UNAWEZAJE KUTIBU SELI ZA MWILI?
Kwa miaka ya hivi karibuni kumetokea mapinduzi makubwa sana kwenye sekta ya afya baada ya kugunduliwa kwa STEMCELL TREATMENTS. Stemcell treatment ni tiba ambayo inalenga kutibu seli za mwili mzima. Unapotumia Stemcell inakwenda kufanya kazi kuu zifuatazo;
1.REJUVENATION
Hiki ni kitendo cha kuhuisha seli ambazo zimelala(dormant) Kazi ya kwanza ya stemcell inapoingia mwilini ina kwenda kuamsha seli zote zilizolala na kuzifanya kuwa hai (active) tena
2.REPAIR
Pia stemcell inafanya kazi ya kurekebisha au kutengeneza seli zilizochakaa au kuharibika. Kwa hiyo kama kuna seli yoyote iliyoharibika jua kwamba utakapoanza tu kutumia stemcell seli hizo zitaanza kurekebishika.
3.REPLACE
Kazi ya tatu ni kuondoa seli zote ambazo zimekufa na haziwezi kurekebishika na hii ndio maana hata kama una kovu utakapotumia stemcell inaboresha muonekano wa ngozi yako yako kwani kovu ni seli ya ngozi iliyokufa.
Kwa hiyo maajabu ya stemcell yamejificha kwenye kazi hizo tatu. Kazi hizo tatu zitakapokamilika basi kinga za mwili wako zitapanda na kupanda kwa kinga za mwili huupa mwili uwezo wa asili wa kufukuza na kuzuia magonjwa kuingia mwilini.
KUNA AINA NGAPI ZA STEMCELL?
Kuna aina nyingi sana kwa sasa za Stemcell ambazo zinatengenezwa na makampuni tofauti tofauti lakini ni muhimu kuelewa kuwa sio zote zina uwezo wa kufanya kazi zote hizo tatu kwa hiyo tumefanya uchambuzi kulingana na research tuliyofanya kwa muda mrefu juu ya Stemcell Treatments. Tumekuwekea aina za stemcell ambazo zinafanya vizuri sana kutibu magonjwa Sugu hasa kwa bara la Afrika.
Dawa hizi hutolewa kwa kuzingatia chanzo cha tatizo, umri wa mtu na ukubwa wa tatizo lilipofikia
Wasiliana na mwakilishi wetu kupitia 0689 310 308. Jibu maswali utayoulizwa kwa ufasaha ili upate tiba inayoendana na tatizo lako.
SEHEMU YA PILI
MATATIZO YA UZAZI KWA WANAUME
Matatizo ya uzazi kwa wanaume yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, na yanahusisha changamoto katika uzalishaji wa mbegu za kiume, usafirishaji wa mbegu hizo, au matatizo ya kimaumbile. Hapa ni baadhi ya matatizo ya uzazi kwa wanaume:
1.Upungufu wa Mbegu (Low Sperm Count): Hili ni tatizo ambapo mwanaume ana idadi ndogo ya mbegu za kiume kwenye shahawa zake. Hii inaweza kusababishwa na mambo kama vile mabadiliko ya homoni, magonjwa ya zinaa, kuathirika na sumu, au matatizo ya kiafya kama vile varicocele (kuvimba kwa mishipa kwenye korodani).
2.Mbegu Zisizo na Afya (Poor Sperm Quality): Mbegu zinaweza kuwa na umbo lisilo sahihi au zisitembee kwa kasi inayotakiwa, jambo ambalo linaweza kuzuia kufikia yai la mwanamke na kulirutubisha.
3.Kutozalisha Mbegu (Azoospermia): Hali hii inatokea pale ambapo mwanaume hana kabisa mbegu kwenye shahawa. Inaweza kuwa kutokana na vizuizi kwenye mirija inayosafirisha mbegu, matatizo ya homoni, au matatizo ya kijenetiki.
4.Matatizo ya Kusisimka (Erectile Dysfunction): Hii ni hali ambapo mwanaume hawezi kupata au kudumisha kusisimka kwa muda wa kutosha kufanya tendo la ndoa. Sababu zinaweza kuwa za kimwili (kama vile magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, au ugonjwa wa kisukari) au za kisaikolojia (mfano msongo wa mawazo, wasiwasi, au matatizo ya kiakili).
5.Matatizo ya Kupiga Shahawa (Ejaculation Problems): Hii ni pamoja na hali kama vile “kuchafua mapema” (premature ejaculation), “kuchafua kwa kuchelewa” (delayed ejaculation), au “kuchafua nyuma” (retrograde ejaculation) ambapo shahawa inaenda kwenye kibofu badala ya kutoka nje.
6. Matatizo ya Maumbile (Structural Problems): Kuna baadhi ya matatizo ya maumbile ambayo yanaweza kuathiri uzazi wa mwanaume, kama vile vizuizi kwenye mirija ya uzazi au maumbile yasiyo ya kawaida ya uume.
7.Magonjwa ya Zinaa (Sexually Transmitted Infections – STIs): Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono au klamidia yanaweza kusababisha uharibifu wa mirija inayosafirisha mbegu na kusababisha utasa.
8.Matatizo ya Homoni (Hormonal Imbalances): Homoni za kiume kama vile testosterone zinapokuwa chini, inaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu na kusababisha tatizo la uzazi.
9.Mtindo wa Maisha (Lifestyle Factors): Matumizi ya sigara, pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya, uzito kupita kiasi, au kuwa na mkazo wa mawazo wa muda mrefu yanaweza pia kuchangia matatizo ya uzazi kwa wanaume.
Kama mwanaume anakabiliwa na matatizo ya uzazi, ni muhimu kutafuta ushauri wa kitaalamu ili kufanyiwa uchunguzi na kupata tiba inayofaa.
Watu wengi wanapopatwa na matatizo haya hufanya kosa la kwenda kununua boosters kama Viagra au Cialis tablets wakidhani kuwa wanatibu tatizo kumbe bila kufahamu ndio wanakuwa wanaongeza ukubwa wa tatizo. Kuna Case ambazo unakuta mtu ametumia boosters mpaka zimekuwa chronic kwenye mfumo wake wa damu kiasi kwamba hata boosters zimefikia mahali zimegoma kufanya kazi na jambo hili hupelekea mtu kuwa na huzuni sana na wengine hufikia hatua ya kujiua kwa kujiona hawana thamani tena mbele ya mwanamke.
Kabla ya kununua dawa yoyote ni vema kwanza kujiuliza tatizo lako limetokana na nini? Kwa sababu bila kujua chanzo cha tatizo utakuwa unatibu dalili tu na baada ya muda tatizo litarudi tena.
Hakikisha unanunua dawa kwa mtu mwenye uelewa wa tatizo hilo kwa kina ili kuepuka kuangukia kwa wafanyabiashara ambao wao wako tayari kuuza kitu chochote ilimradi tu wapate pesa.
Upungufu Wa Nguvu Za Kiume
Upungufu wa nguvu za kiume, au erectile dysfunction (ED) kwa Kiingereza, ni hali ambapo mwanaume hawezi kudumisha au kupata nguvu za kutosha za kuweza kufanya tendo la ndoa. Sababu za upungufu wa nguvu za kiume zinaweza kuwa za kisaikolojia, kimwili, au mchanganyiko wa vyote viwili.
Jinsi Ya Kutibu Upungufu Wa Nguvu Za Kiume
Hatua Ya Kwanza
Hatua ya kwanza ni kutambua tatizo lako limesababishwa na nini hii itakusaidia sana kufanya maamuzi sahihi juu ya tiba gani utumie. Baadhi ya wanaume wamejikuta kwenye tatizo hili kutokana na tabia ya kuchua sana (masturbation), wengine ni kuwa na unene uliopitiliza,wengine maradhi kama kisukari na pressure,wengine ni kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara,wengine ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kali au yaweza kuwa ni matatizo ya kisaikolojia. Kwa hiyo kutambua tatizo lako limetokana na nini ndio sehemu ya kwanza kwenye tiba.
Kwa mfano….
Ukishajua kuwa tatizo lako limetokana na kujichua, unatakiwa kwanza uache huo mchezo kabla hata ya kuanza kutumia dawa au unapotumia dawa hakikisha umeacha kabisa mchezo wa kujichua laa sivyo kama unatumia dawa huku unaendelea kujichua basi wewe kupona itakuwa ngumu. Vivyo hivyo rekebisha kila sehemu katika maisha yako,hakikisha unafanya mazoezi,unapata mlo kamili,hakikisha unapata muda wa kutosha kupumzika na pia fanya kila unaloweza kupunguza stress.
Hatua Ya Pili
Hatua ya pili ni kuhakikisha unatibu kwanza magonjwa mengine kwenye mwili kabla ya kutibu nguvu za kiume. Kwa mfano mara nyingi tatizo la upungufu wa nguvu za kiume huweza kusababishwa na magonjwa mengine kama kisukari kwa mfano. Inaeleweka kuwa wanaume wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari pia hukabiliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na hii pia hutokana na matumizi ya madawa makali ya kupunguza ukali wa ugonjwa husika. Pia kuna magonjwa kamba vidonda vya tumbo,bawasiri na tezi dume pia hupelekea mtu kushindwa kuwa imara kwenye tendo la ndoa.
Ushauri Wangu……
Kwa sababu watanzania tulio wengi hatuna utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya wa mara kwa mara hivyo basi inaweza kuwa ngumu kujua ni magonjwa mangapi unayo kwenye mwili kwani kuna baadhi ya magonjwa huwa hayaonyeshi dalili mpaka ugonjwa ufikie kwenye hatua mbaya,kwa hiyo ushauri wangu ni kwamba kama unajijua hauna utaratibu wa kafanya uchunguzi wa afya wa mara kwa mara ni vema kutumia STEM CELL. Stemcell itakusaidia kutibu magonjwa yote yaliyopo mwilini mwako yani unayoyajua na usiyo yajua,lakini pia itakusaidia kupunguza gharama za matibabu kwani kuna baadhi ya vipimo ni gharama sana na vinachukua muda mrefu. Kufahamu zaidi kuhusu Stemcell treatment rudi kusoma sehemu ya kwanza hapo juu.
Hatua Ya Tatu
Hakikisha unatengeneza tabia ya kufanya mazoezi hasa yale yanayosaidia kuongeza mzunguko wa damu kwenye prostate area ka kama mazoezi ya kegel. Mazoezi yatakusaidia kuondoa sumu,kupunguza stress na kukuongezea stamina. Hta kama unatumia dawa ni muhimu kuendelea na labda kama unaumwa au una udhaifu wowote wa kiafya
Dawa hizi hutolewa kwa kuzingatia chanzo cha tatizo, umri wa mtu na ukubwa wa tatizo lilipofikia
Wasiliana na mwakilishi wetu kupitia 0689 310 308. Jibu maswali utayoulizwa kwa ufasaha ili upate tiba inayoendana na tatizo lako.
SEHEMU YA TATU
MATATIZO YA UZAZI KWA WANAWAKE
Matatizo ya uzazi kwa wanawake ni mambo yanayoweza kuathiri uwezo wao wa kushika mimba au kuzaa mtoto mwenye afya. Haya matatizo yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu, na yanasababishwa na sababu mbalimbali. Hapa kuna baadhi ya matatizo ya uzazi yanayoweza kuwakumba wanawake:
1.Matatizo ya Ovulation: Hii inahusisha kutokuwepo kwa ovulation au ovulation isiyo ya kawaida, ambayo ni sababu kubwa ya utasa. Polycystic Ovary Syndrome (PCOS) ni tatizo linaloathiri ovulation na linaweza kusababisha uzazi wa shida.
2.Matatizo ya Mirija ya Fallopian: Ikiwa mirija ya fallopian imeziba au imeharibiwa, yai linaweza kushindwa kufika kwenye uterasi kwa ajili ya urutubishaji. Matatizo haya yanaweza kusababishwa na maambukizi, upasuaji, au magonjwa kama vile Pelvic Inflammatory Disease (PID).
3.Endometriosis: Ni hali ambapo tishu zinazofanana na zile zinazopatikana kwenye ukuta wa ndani wa uterasi (endometrium) hukua nje ya uterasi. Hii inaweza kusababisha maumivu makali na kuathiri uzazi.
4.Matatizo ya Uterasi: Shida kama vile fibroids (uvimbe wa misuli ya uterasi), polyps, au kasoro za kuzaliwa kwenye uterasi zinaweza kuathiri uwezekano wa kushika mimba au kuendelea na ujauzito.
5.Matatizo ya Shingo ya Kizazi (Cervix): Matatizo kwenye shingo ya kizazi, kama vile kuziba au hali ambapo shingo ya kizazi haiwezi kufunguka wakati wa kuzaa (cervical insufficiency), yanaweza kusababisha ugumu wa kushika mimba au kupoteza mimba.
6.Magonjwa ya Homoni: Magonjwa kama vile hypothyroidism au hyperthyroidism yanaweza kuathiri uzazi kwa kuingilia kati mzunguko wa hedhi na ovulation.
7.Matatizo ya Mfumo wa Kinga (Immunological Disorders): Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na matatizo ya kinga yanayofanya mwili kushambulia tishu za uzazi au mimba yenyewe.
8.Umri: Kuongezeka kwa umri, hasa zaidi ya miaka 35, kunaweza kupunguza uwezo wa uzazi kutokana na kupungua kwa idadi na ubora wa mayai.
9.Matatizo ya Maumbile (Genetic Disorders): Baadhi ya matatizo ya maumbile yanaweza kuathiri uzazi, kama vile Turner syndrome au Fragile X syndrome.
10.Matatizo ya Kisaikolojia na Kimazingira: Stress, lishe duni, uzito kupita kiasi au upungufu wa uzito, na matumizi mabaya ya pombe au dawa za kulevya zinaweza pia kuchangia matatizo ya uzazi.
Matibabu ya matatizo ya uzazi hutegemea sababu na yanaweza kujumuisha dawa, upasuaji, au teknolojia za uzazi msaidizi kama vile IVF (In Vitro Fertilization). Ni muhimu kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi kushauriana na daktari kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi.
P.I.D(Pelvic Inflamatory Diseases)
PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni ugonjwa wa maambukizi unaoathiri viungo vya uzazi vya mwanamke, kama vile mji wa mimba (uterasi), mirija ya uzazi (fallopian tubes), na ovari. Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na bakteria wanaoingia kwenye viungo vya uzazi kupitia njia ya uke, hasa kupitia maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na klamidia (chlamydia).
Dalili za PID
– Maumivu ya tumbo la chini au kiuno.
– Kutokwa na uchafu usio wa kawaida kutoka ukeni.
– Maumivu au kutokwa na damu wakati wa kujamiana.
– Maumivu wakati wa kukojoa.
– Homa au hisia ya baridi.
Madhara ya PID
– Ugumba (infertility) kutokana na uharibifu wa mirija ya uzazi.
– Maumivu sugu ya nyonga.
– Uwezekano mkubwa wa kupata mimba nje ya mji wa mimba (ectopic pregnancy).
– Maambukizi ya mara kwa mara kwenye viungo vya uzazi.
Dawa hizi hutolewa kwa kuzingatia chanzo cha tatizo, umri wa mtu na ukubwa wa tatizo lilipofikia
Wasiliana na mwakilishi wetu kupitia 0689 310 308. Jibu maswali utayoulizwa kwa ufasaha ili upate tiba inayoendana na tatizo lako.
Featured Products
-
Sh 65,000Original price was: Sh 65,000.Sh 60,000Current price is: Sh 60,000.Vidonge vya Powerful Luxury Glutathione Extra Whitening Capsules hutoa mng’ao...
-
Sh 80,000Original price was: Sh 80,000.Sh 75,000Current price is: Sh 75,000.Joint Support Capsules for Bone and Joint Flexibility -100% Effectively ...
-
Sh 55,000Original price was: Sh 55,000.Sh 50,000Current price is: Sh 50,000.Alpha Brain Focus Energy Shot - Brain Booster ya Haraka...
-
Sh 55,000Original price was: Sh 55,000.Sh 50,000Current price is: Sh 50,000.Elderberry with Zinc and Vitamin C Capsules - 100% Effective...